7. Machi 2024

Permaculture ( Kilimo cha muda mrefu )

Ingawa Kilimo ya kawaida hutumia kemikali ambazo huuwa vijidudu vidogo ambavyo huishi kwa mchanga, permaculture au kilimo cha muda mrefu- kwa upande mwingine inafanya kazi pamoja na vijiduduu hivi kuikuza ardhi. Kwa mfano, njia moja ya kukuza ardhi hii ni kwa kupanda miti. Katika njia hii, mchanga unawachanawachana halafu maji inaweza kunyunyika virahisi.

Mojawapo ya kanuni ya permaculture ni kwamba mtu mmoja hawezi kujua kila kitu.  Kila mmoja anasambaza elimu na wengine na pia anafunzwa mambo mengine kutoka kwa wengine na hatimaye kila mtu ataweza kupata maarifa kamili kuhusu permaculture. Njia hii pia inakuza imani kwa wahusika wote.

Kanuni ingine ni kwamba kila mtu anajiunga na kazi hii ya permaculture, kuanzia mavuno, kusambaza mimea na hata katika kutengeneza maamuzi ya mboga au matunda ambazo zitapandwa.  Watoto nao pia wanapata elimu ya kukuza ardhi na rasimlimali wakiwa bado wachanga. Ili familia zote ziweze kuhusika, familia ambazo wana watoto wadogo wanasaidiwa kulea watoto hawa,  ili wazazi nao waweze kuhusika katika jamii.  Lengo haswa ni kuwa kila mmoja katika jamii anachangia kwa uwezo wao mdogo na hatimaye unakuwa ni mchango mkubwa. Permaculture ni mradi wa amani.