3. Novemba 2024

Elimu / Mafunzo

“Elimu sio njia yakuepuka umaskini , ni njia ya kupigana nao.” (Julius Nyerere)

Elimu ya maendeleo endelevu huzingatia umuhimu wa kuweza kukuza na kutimiza suluhisho ambazo zitasaidia jamii kuendelea mbele kwa njia ya kuweza kujidumu kama jamii na pia kibinafsi.

Ili  kukuza shamba lililoko Fukayosi, Tanzebras wanataka kuiga mbinu wa ”didactic” ambayo inafunzwa katika kituo cha Practical Permaculture ya Afrika mashariki. 

Kutokana na mpangilio wa uwanja hadi kuchagua mimea ambayo itapandwa na kuvunwa na hatimaye kuuzwa, vijana wanastahili kuelimika kutumia vyombo ambavyo vitawasaidia katika maisha yao ya kitaalamu. Tungependa kuwatuma wanafunzi katika kituo hicho kule Zanzibar ili nao wapate mafunzo haya. Kwa vile hatuwezi kuwatuma watoto na vijana wote, watakaoenda kwa muda wa wiki mbili, wataweza kusambaza elimu ambayo watapata huko na wenzao watakaporudi  Gongo la Mbotoni. Hilo ndilo lengo letu kuu la kupigana na umaskini, mwalimu Julius Nyerere alivyonukuu.

Hatutaki tu kufunza vijana hawa, bali tungependa pia kuwasaidia katika ukuzaji wa maisha yao kijumla. Na ndiyo maana ni muhimu sana kwetu iwapo wanafunzi hawa wataweza kuwaelezea wenzao yote ambayo watasomea. Udumishaji wa permaculture inapasa kuwa na athari ambazo zitadumu, kuelimishana pamoja na pia kutumia vifaa kwa njia ya heshima. Elimu ya hali ya juu ni muhimu ili malengo yote yataweza kufanikiwa, malengo ambayo pia tunafwatilia  katika mahusiano yote.

Ili mambo haya yaweze kufanikiwa, itabidi watu waje pamoja na waketi ana kwa ana. Je, ungependa kuungana na kusaidia Tanzebras katika miradi yao au hata kuwatembelea?

Tuelezee matarajio yako au maoni yako kupitia : info-reisen(at)tanzebras.com.

Tutafurahia sana kuwaona!