3. Machi 2024

Tunasema kwaheri Peter

Siku ya Alhamisi, tarehe 12 Machi, tulipokea habari ya kuhuzunisha mno ya kwamba  Hessenzebra wetu, alias Peter Routhier,  aliaga dunia baada ya kupambana na ugonjwa wake wa saratani. Ilikuwa ni mwezi uliopita tu ambapo tulituma matakwa yetu ya kupona katika video hii fupi :
Sisi kama TanZebras, ambao tulijiunga na mpango wa bima ya afya kupitia kampeni ya mashabiki wa MSV, tunaelewa kinaganaga uchungu wa kufiwa katika mahusiano muhimu haswa ya kijamii. Vijana wengi hupoteza wazazi wao wakiwa bado wachanga na inabidi jukumu la kulindwa na kukuzwa liendee akina ndungu na jamaa ya familia.
TanZebras, ambao wanajiona kama familia ya MSV, tungependa nasi pia kutuma rambi rambi zetu kwa familia ya Peter na haswa kwa mkewe Angie na mwanawe Patrick.

 

R.I.P. Peter

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *