13. Septemba 2024

Mechi iliyoairishwa dhidi ya Dar Star FC ya isha bure kwa bure

Mechi dhidi ya Dar Star FC iliweza kuchezwa hatimaye baada ya T.F.F. kuiairisha, kwa sababu Marefa walichelewa kufika katika hatua ya kwanza.

Wakati ulifika na Timu yetu ilihofia ushindi huu muhimu. Angalau pointi moja kwa timu hizi mbili ilikuwa ni lazima. Wote waliweza kuing’ang’ania kwa udi na uvumba. Mchwano huu mkali ukawa unachezwa kati kati ya uwanja. Nafasi za kutinga mabao ukazidi kuwa nadra katika upande zote.

Hata baada ya mapumziko, timu zote mbili hawakufanikiwa kupata nafasi hatari za kufunga mabao. Nahodha  wa timu yetu Franco, aliyeanza mechi kwa matumaini, alifiwa moyo, hakuna asiyeweza kumuhimiza.

Baada ya mechi hii iliyoairishwa, Tanzebras sasa wako katikati ya ligi, huu ukiwa mafanikio mazuri kwao.

Mpinzani ujao utakuwa FC Karume Market na baadaye Airwing ambao wanatangulia kwenye ligi.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *