MATCH REPORT (KARUME FC VS TANZEBRAS FC)
Ni mechi ya mwisho ya kundi A katika ligi daraja la 3 ambayo ilizikutanisha timu ya Karume FC vs TanZebras FC. Mchezo ambao ulikua mgumu sana kutokana na timu ya Karume FC kuhitaji alama moja tu ili iweze kufuzu hatua inayofuata lakini kwa upande wa Tanzebras FC ulikua ni mchezo wa kukamilisha ratiba tu. Ni mechi ambayo iliteka hisia za mashabiki wengi wa soka kutokana na timu mbili zilizokua zikipambana lakini pia ni mchezo ambao ulikua unaamua hatma ya kundi A.
Karume walianza mechi hii wakiwa na presha kubwa wakitafuta goli la mapema,lakini Tanzebraswalionekana kua bora katika safu ya ulinzi kuweza kuwazuia Karume wasiweze kupata goli la mapema. Kuanzia dakika 25 TanZebras walianza kuonekana wakiutawala mchezo huo na kupiga pasi nyingi sana huku Karume FC wakionekana kuzidiwa kimchezo,Licha ya kutawala mchezo huo TanzebrasFC hawakuweza kupata bao la kuongoza.
Baadae dakika ya 30 Timu ya karume FC walitangulia kupata goli la uongozi wa mchezo huo,bao hilo liliofungwa kwa njia ya mpira uliopigwa krosi na kumfikia mshambuliaji wao na kupiga shuti kali lililoingia moja kwa moja golini.
Lakini dakika 12 baadae TanzebrasFC waliweza kusawazisha goli hili kwa mkwaju wa penalty iliyifungwa kwa ufundi mkubwa na mzhambuliaji JORDAN MLANDA na kufanya matokeo kuwa KARUME 1-1 TANZEBRAS
FC mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi zaidi huku kila timu ikitafuta ushindi lakini KARUME FC walionekana kuwa bora zaidi TanZebras FC,hatimaye dakika ya 60 na 78 karume waliongeza mabao mawili ambayo yaliweza kuwafanyawawezekupata ushindi wa jumla ya mabao 3-1 hivyo kuwafanyawaweze kufuzu hatua inayofuata.lakinikwa upande wa Tanzebraskuendelea kusalia katika ligi daraja la 3 ambayo itaendelea tena mwakani.
MANENO YAKOCHA DAUDI BAADA YAMECHI
“Tunajua matokeo haya sio mazuri kwetu lakini pia kwa mashabiki zetu ila ndo mchezo ulivo,Tulijitahidikupambana kwa kiasi kikubwa ila wakati mwingine matokeo ya mchezo huja tofauti.Ni msimu wetu wa kwanza katika ligi tumejifunza mengi naamini tutafanya vizuri zaidi msimu ujao,Nawashukuru mashabiki zetu kote duniani kwa support yao kubwa wanayotupatia na tuna waahidi kufanya vizuri msimu ujao” COACH DAUDI
MANENO YAMANAGERWA TIMU DON BAADA YAMECHI
“Timu yetu ni bora imepambana kwa kiasi kikubwa na imeleta mapinduzi katika ligi daraja la 3 watu wengi wanaifuahia ingawa hatujafanikiwa kufuzu hatua inayofuata,Huu ni msimu wetu wa kwanza katika Ligi daraja la 3 ulikua ni msimu mgumu lakini naamini tumejifunza mambo mengi ambayo tutayafanyia kazi kwa ajili ya msimu ujao, Tuna washukuru wachezaji wote na watu wote wanaotusapoti kote duniani asanteni sana.” TEAM MANAGER DON