13. Septemba 2024

Bima na Mikataba – Kazi ya Ofisini yaleta raha kweli!

 

April 2020: Corona yatia dunia nzima katika hali ya wasiwasi.  Uropa ipo katika hali ya hatari. Soka kote umeghairishwa. Iwapo wachezaji wanaweza kucheza, mashabiki nao hawaruhusiwi kuingia kwenye viwanja vya michezo. Lahaula lastaflahi!

Kuelekea Kusini, kule Gongo La mboto, eneo la Dar Es Salaam, Tanzania, Don ana mawazo mazuri ya kulisajili Tanzebras, timu ya soka ya mtaani, katika  Shirikisho  la Soka nchini (TFF). Motisha ulioje!

Habari hii inatia wahusika ambao wako Duisburg, kilometa 7000 mbali, katika hali ya  uoga na wasiwasi. Mradi huu ambao ulianza kimchezo tu, sasa unastahili kutimizwa. Wachezaje wanakosa vifaa kadha wa kadha ambazo ni za muhimu katika mchezo huu. Hawana Bima iwapo kuna majeraha, mikataba ambazo zitawajumuisha na kilabu. Mbali na hayo hakuna fedha za kulipia leseni au hata kulipia michezo. Ingawa chombo cha habari kupitia facebook uliandaliwa, huu haungetosha kutumika kwa msimu mzima.

MSVPortal tena ukawa ni mtandao mwafaka kwa wanazebras. Kwa mda mfupi tu mashabiki wa nguvu walikusanyika na kutayarisha tovuti na fedha za bima ya watoto 60 pia ulikusanyiwa. Fedha hizi ziliweza kununua bima ya misimu mitatu. Msaada wa kisheria pia haukusahaulika, ambapo wachezajiwaliweza kupata mikataba kulingana na sheria za FIFA na TFF.

Sasa baada ya miezi misita, wakati ulifika ambapo wajumbe wa kampuni ya Bima walikuja ofisini  mwa Tanzebras (nyumba ya Don ulipangwa vizuri ukawa ndiyo ofisi za Tanzebras) ambapo vyeti vya kilabu vya watoto uliletwa na watoto kupewa. Fedha nazo zilikuwa zimeshawasili hapo awali. Mikataba za wachezaji nazo zilitiwa sahihi na zinginezo kuhalilishwa na alama za vidole.

 

  

Ofisi Nyumbani kwa njia tofauti

 

Jezi mpya nazo zilichapishwa majina.  Sasa nikuwinda ma punkti tu!

   

Maombi kabla ya mechi!

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *