Jumamosi, Oktoba 17, 2020 Tanzebras waalikwa katika Nafasi Art Space. Siku hii ilifaa kuwapea watoto nafasi katika zanaa za maonyesho. Nafasi Art Space ulianzishwa mwaka wa 2008. Hapo awali ilikuwa ni kikundi kidogo cha wasanii wa Tanzania. Leo imekuwa ni jamii kubwa ya wasanii, wanamuziki, wanasarakasi na mafundi kadha wa kadha katika eneo la viwanda kule Mikocheni B, Dar es Salaam .
Jukwa la Nafasi Art Space imewapa wasanii uwanja wa kukuza usanii na kupea vijana watanzania nafasi ya kukuwa wanabiashara katika usanii na utamaduni.
Kikundi cha wanatanzebras hamsini (50) waliweza kutembelea Nafasi kwa mara ya kwanza. Asubuhi hiyo , wanatanzebras waliweza kutambulishwa katika dunia ya usanii na Jesse Gerald, meneja wa miradi wa zanaa za maonyesho, Nafasi. Aliwaelezea kuhusu waanzilishi wa Sanii Tanzania kama vile Prof. Elias Jengo, Raza Mohamed, Sam Ntiro and Edward Tingatinga. Watoto waliweza kuwauliza hawa waanzilishi maswali kadha wa kadha. Baadaye watoto waliweza kuzuru na kutazama maonyesho katika vyumba tofauti. Walidukuu pointi na pia waliruhusuwa kupiga picha.
Wanatanzebras wetu waliweza kushiriki katika warsha mbili: Katika moja yao, waliweza kuzungumza mambo ya utamaduni wa kupiga ngoma na historia ya densi kutoka mikoa kadhaa ya Tanzania,. Walielezwa pia maana halisi ya kila densi, wakati na mahali densi hizi hutendeka, na pia wakaweza kuonyeshwa densi hizi.
Warsha hii iliongozwa na Shine Dance Group.
Warsha ya pili uliongozwa na Anthony Hall (aka Grandpa Stork), Mwamerikani ambaye anahusika na njia za mafunzo ya watoto, kupitia mazoezi.
Baada ya mafunzo hii asubuhi, mapocho pocho kadha wa kadha uliandaliwa kwa walioshirikia, kama vile matunda na samosa. Baadaye wakaenda katika warsha ya usanii wa Grafiti, uliyoongozwa na Andrew Munua. Matokeo yakawa ni maandishi ya Zebra kwa rangi ya samawati. Hatimaye watoto waliweza kuwatumbuiza na wimbo wa Tanzebras na pia wakaweza kuigiza densi mpya ambalo walifunzwa.
Hatimaye kundi hilo likarudi Gongo la Mboto saa kumi hivi.
Watoto wa Tanzebras walihusishwa siku nzima, nyuso zao zilijaa furaha mpwito mpwito.
Sura zao hazingeweza kuficha hiyo furaha katika mapicha na video zilizochukuliwa siku hiyo.
Waandalizi wa Nafasi walifurahishwa sana na kundi hilo la Tanzebras ambao, wakasema walikuwa wamejiandaa vizuri na pia waliweza kuona undugu ambao upo katika kundi hilo na wote ni familia moja kubwa.
Here a comprehensive picture gallery of the day – have fun with the impressions: