3. Machi 2024

Msaada Umewasili!

Baada ya miezi kadhaa, mashabiki wa timu ya MSV Duisburg walifanya michango ili kununulia Tanzebras vifaa. Hapo mwanzoni wa mwaka, viatu na mipira viliwasili Gongo la Mbotoni, na hatimaye, katika mwezi wa Agosti, majezi, mashati, koti na vifaa tofauti tofauti kama vile hata saa ya ukutani wa timu ya MSV na mtakasaji wa maji kutoka whatabird nazo pia zilifwata.

 

 

Katika tukio hilo ambapo Mathias na Jörg walikuja kupeana vidhaa hivi, sherehe ndogo ulitayarishwa ambapo mapochopocho kadha wa kadha ukaandaliwa. Vifaa hivi vikafunguliwa, kaguliwa na hatimaye kugawanywa kwa kila mwanachama!

 

Bila shaka jezi mpya nazo pia zilipimwa papo hapo. Jezi za MSV -msimu wa 2019/2020 ukawa ndio kilele cha siku hii!

 

Tungependa sana kuwashukuru wafadhili wetu kwa moyo mkunjufu. Katika wakati huu mgumu wa Corona, bado waliweze kujitolea kwa kutupea zawadi hizi.  Tukio hili limetugusa moyoni na tumefurahia sana kuwa na marafiki kule Duisburg ambao wameweza kufanya haya mambo yote mazuri kutendeka.

 

 

Asante sana!

 

 

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *