8. Oktoba 2024

Paradiso ndogo kwa wana TanZebras!

 

Je ungependa kushirikiana nasi kwenye uanzilishaji? Jiunga nasi katikaTanzebras Adventkalenda 

 
Wakati uo huo waweza kujishindia mojawapo ya zawadi kubwa au ndogo ambazo zimefichikia katika milangi hizi 24!
 
Pesa hizo ambazo zitakusanyiwa katika kalenda hii, zitatumika kununua mbegu ambazo mwishoe zitaleta mivuno chunguu tele, katika misimu yote ya mwaka.
 
Ndizi, mananasi , maembe, tikiti maji, vitunguu, viazi vitamu na mimea mengine mengineyo ni mifano ya mimea ambazo zitapandwa katika hekari mbili ya shamba mwanzoni mwa mwaka ujao – 2021.
 
Kupitia msaada wenu, tungependa kuwapea wanaTanzebras uwezo wa kujitegemea kimaisha katika msimu huu wa Krisimasi kwa njia ya permaculture  ya matunda na mboga

 

 

    

Ukitizama Afrika Mashariki sasa hivi, kuna maswala nyeti na mahangaiko katika sekta kadha wa kadha: Watu kufutwa na kupoteza kazi, familia zingine huenda wakalala njaa kwa sababu ya ukosefu wa chakula. Kwengineko familia nyingi wameathirika na tauni hii.

Ingawa Tanzebras wana mafanikio mengi katika soka, ni muhimu pia wawe na mafanikio zaidi katika uwanja zingine tofauti. Kupitia njia hii wanaweza kujitegemea ikija eneo ya kujilisha na kujidumu. Hatimaye itakuwa ni mafanikio zaidi ata kuliko hiyo ya uwanja wa mpira!

 

Kuanzia Desemba tarehe 1,Mlango mmoja utafunguliwa kila siku na mshindi kutangazwa hatimaye. Kama mfadhili, utaingizwa katika mashindano ya zawadi hizo 24. Kwa kila  5€, nambari ya mchango wako utawekwa kwenye mchezo wa bahati nasibu. Kwa mfano, ukichanga 20€, bahati yako inaongezeka mara nne kwa sababu nambari yako ya mchango umeingizwa mara nne.

 

Video mbili za Inka na Moses ambazo zinonyesha maana halisi ya kila mchango mdogo!

Kufikia sasa kuna michango ya Adventkalenda ya 1,380€.
 
Asanteni sana!
 

 

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *