3. Machi 2024

Ujenzi wa Kisima yakamilishwa

 

Ujenzi wa Kisima shambani umekamilika.  Maandalizi ya udongo yatafanyika katika siku chache zijazo kabla ya miche kupandwa na Utamaduni wa Kilimo cha muda mrefu (Permaculture) hatimaye kung’oa nanga.Ubalozi wa Ujerumani unaunga mkono mradi huo kwa kiwango cha tarakimu tano. 

 

Hii ni hatua nyingine ambayo itawasaidia wanatanzebras kujisimamia. Katika shamba hilo ambalo NGO ya Planet Hope lilimiliki tangu mwaka 2017, kisima cha mita 110 limeweza kuchimbwa kupitia msaada wa  Ubalozi wa Ujerumani jijini Dar es Salaam, ambao uliunga mkono mradi huo kwa kiwango cha Euro 10,000. Kisima hicho  kinaendeshwa na mfumo wa jua na kina uwezo wa kuhifadhi lita 5,000 ya maji. Kwa upande wa uendelevu wa kiikolojia, matumizi ya nishati mbadala yalikuwa ya umuhimu haswa kwetu.

 

 
 Familia ya Zebra yaweka msingi wa ufadhili 

Ili kukidhi mahitaji ya ufadhili, ilitubidi tudhibitishie ubalozi kuwa mtaji wa usawa kiasi cha asilimia 15 ya jumla unaweza kuibuliwa kutoka kwa fedha zetu . Tungependa kutoa shukrani zetu maalum kwa mashabiki wote wa MSV na wafuasi wengine ambao ukarimu wao ulitoa mchango wa uamaamuzi!

Hatua itakayofwata ni kuandaa shamba. Udongo lazima ulimwe na mifereji kwa ajili ya umwagiliaji wa maji kuandaliwa. Katika majira ya kuchipua, upandaji katika takriban hekta mbili unaweza kuanza. Miche na mbegu ambazo  zinazohitajika zilifadhiliwa katika msimu wa Krismasi kupitia Adventkalenda mtandaoni. Jumla ya euro 5,000 iliibuliwa na Zebraherde e.V. na wafuasi wengi zaidi.

 
Mbinu ya multilayered inafuatiliwa 
 

 Wanatanzebras wawili waliweza kuhudhuria semina ya vitendo juu ya kilimo endelevu katika Taasisi ya Permaculture ya Afrika Mashariki-Zanzibar Kupitia mchango zaidi, miongoni mwao kuwa wadhamini wetu Re-Match kutoka Denmarki. Maarifa ambayo wachezaji wetu Franco na Sophia walipata yataweza kutumika shambani.

 

Kuanzia mananasi, mihogo (manioc) na hatimaye aina kadha wa kadha za mboga na matunda zitapandwa  Gongo La Mboto, nyumbani mwa wanatanzebras. Baadhi ya mimea hii itawanufaisha wachezaji na familia zao, huku mengine yakiuzwa madukani na mikahawani  jijini mwa Dar es Salaam, ili kuhakikisha timu zetu ziweze kuendelea kucheza.
 
Tungependa kuchukua fursa hii kuwashukuru tena, kutoka chini mwa mioyo yetu, marafiki na walinzi wetu wote kutoka bara hizi mbili,  ambao wanasaidia kuendeleza mradi huu wa kipekee wa mpira wa miguu .

 

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *