Familia ya TanZebra inaomboleza kifo cha Furaha (”Happy” kwa Kiingereza). Furaha alikuwa na miaka 15 tu, alipoaga dunia usiku wa kuamkia leo, wa sababu ya shida ya moyo wake.
Malkia wetu wa kwanza anaacha shimo kubwa sana katika jamii yetu.
Furaha, ulikuwa msichana wa kwanza aliyedhubutu kucheza mpira uwanjani na wavulana ingawa hamkuwa sawa.
Kila wakati ulikuwa katika mstari wa kwanza. Ulishiriki katika shughuli zote, iwe ubalozini au katika kituo cha sanaa cha Nafasi. Ulijitolea bure kwa udadisi wako.
Uadilifu wako na ustaha wako ulituvutia na ulikuwa mfano mwema. Tabasamu lako lilikuwa ni ishara ya jina lako.
Kamwe hatutokusahau. Pumzika kwa amani.
Daima utakuweka katika mioyo yetu!
Hivi ndivyo utabaki katika mioyo yetu!
One thought on “Tunaomboleza kifo cha Furaha!”