8. Oktoba 2024

Tamasha la Eid Mubarak

Huku msimu wa Ramadan ulipofika mwisho, Familia ya Tanzebra iliweza kukuja pamoja ili kusherehekea Eid Mubarak kama familia moja.
 
Watoto wote, karibu mia moja pamoja na familia zao walialikwa kwenye tamasha hili la kuvutia , ambapo kulikuwa na kucheza densi nyingi 
na sherehe chungu nzima. Padri aliyewakilisha wakristo, pamoja na Imamu aliyewakilisha waislamu walikuwepo, ambao kwa upande wao walisifia sana miradi ya Tanzebra na kazi nzuri ya kuleta jamii tofauti tofauti pamoja.
 
Baadaye wachezaji walituzwa medali na Kocha wao Martin Hammel, kwa kazi yao nzuri katika timu, kama vile kukuwa na nidhamu bora. Sherehe hizi pia ilichapishwa magazetini, ambapo Farida Abdalla na  Kelvin Mazika pia waliwezwa kutajwa magazetini, kwa  majukumu yao makubwa katika kazi ya timu, kwa kuwaleta watoto na familia zao pamoja. 
 
Kulikuwa pia na zawadi ndogo kwa kila mtu (chupa ya kunywa ambalo lina jina la Tanzebra kwa ajili ya michezo) na hatimaye muziki na densi kwa wingi. 
Wimbo wetu wa Tanzebra nalo likaimbwa moja kwa moja. Tukio hili pia liliashiria maadhimisho ya maisha ya mmoja wa 
wachezaji wetu, Furaha ambaye aliaga dunia akiwa na miaka 15 tu . (angalia makala iliyopita hapa). Wimbo ambao uliandikwa kama kumbukumbu lake pia iliimbwa. 
 
Baadaye alikuja DJ, ambaye alikipasha moto sherehe hizo, ambapo Tanzebras waliendelea kusherehekea Eid kweli kweli.

 

 

 

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *