2. Machi 2024

Nick , zawadi ya Pasaka

 
 
Kabla ya Nick VI. kufunga safari ya kuelekea uwanja wa ndenge wa Düsseldorf , aligonga mlango wa TanZebras FC, kwasababu angependa kuwatembelea  akiwa katika ziara zake kule Tanzania.
 
 Kutokana na habari hii njema, wazo likazua punde hii, kwamba Nick angeweza kubeba vifaa kadhaa wa kadhaa na kuvileta Tanzania.
 Kwa bahati nzuri kulikuwepo tayari masanduku machache ya michango ambayo yalikuwa  katika karakana ya marion kwa muda. 
 
Bila kupoteza wakati, sanduku iliyojaa mipira ya Derby-Star na viatu vipya vya Soka , ambavyo vilikuwa vimefadhiliwa na “Team Lechti” , vilisafirishwa moja kwa moja mpaka uwanja wa ndege wa Düsseldorf. Katika hatua hii, tungependa sana kumshukuru shabiki wa VfL Bochum, Markus G. kutoka Neudorf na bila shaka kumshukuru Marcel na sungura wake mdogo. 

 
Mara tu Nick alipotua Tanzania, alipanga kukutana na Don kwa ajili ya makabidhiano ya mizigo hii. Bila shaka hatua hii iliwapa wachezaji wetu furaha na nafaka isiyo na mipaka, na siku hiyo ikawa ni siku ambayo haitosahaulika kamwe!  Si ajabu kwamba picha hizi nzuri na za kuvutia zilichukuliwa:

 

 

 

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *