9. Disemba 2024

Mashindano ya Krismasi yafua dafu – Sehemu ya kwanza

 
Katika kipindi cha mwisho cha Krismasi, tulitoa kalenda maaluma mbapo tuzo 24 ziliweza kushindwa. Mshindi mmoja, alikuwa ni Kathrin kutoka Duisburg; ambaye angeweza kuhudhuria  ziara ya ”Kiez-Tour” pale St. Pauli.
 
Sasa kila kitu kilikuwa kimeandaliwa na Sigi, TanZebra wetu kutoka kule kaskazini, ambaye alikuwa tayari kumuonyesha Kathrin na rafiki yake Silke
makala maalum ya jiji la Hamburg.
 

Ifuatayo ni taarifa ya washindi hao, pamoja na mapicha:

Advent kalendar ya Tanzebras– Ziara ya Kiez Tour kupitia St. Pauli

“Katika mwangaza mkali wa jua katika Landungsbrücken, tulipatana na Sigi saa 11:20 asubuhi. Aliweza kutambulika mara moja, na papo hapo tukaambatana moja kwa moja ili kuizuru jiji la Hamburg.
 
Tulitembelea vituo vyengi vipya ambavyo kama mtalii hungeweza kugundua. Tuliweza kuona St. Pauli katika mtazamo tofauti. Maswali yetu yote kutoka Cologne na Duisburg yaliweza kujibiwa kinaga ugabaga kwa uvumilivu.
 
Baadaye tulikuwa na fursa ya kushuhudia mwanzo wa ligi pale FC ST. Pauli katika uwanja wa mpira wa Millerntor.

 

Tungependa kumshukuru Sigi kwa wakati wake, na kwa kutufunza mambo mengi kuhusu St Pauli.

Tutafurahia sana iwapo tutaweza kurudi  hapa tena.

Salamu chungu nzima kutoka Kathrin na Silke !

 

Bila shaka tunafurahia kwamba mnazidi kuungana  mikono na sisi katika miradi yetu. Asanteni sana na tunatumai kuwaona tena, iwe ni St. pauli, au katika uwanja wa mpira wa Wedau au hata Tanzania.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *