2. Machi 2024

Mashindano ya Krismasi yafua dafu – Sehemu ya pili

 
Sio tu kwamba kulikuwa na tuzo za kushinda, lakini michango iliyozalishwa iliweza kutumika kujenga nyumba kwenye shamba letu ndogo .
 
Baada ya kuchimba kisima,  na uwezo wa kutumia umeme  kutokana na nishati ya jua ambayo ulikuwa ni msaada kutoka kwa Ubalozi wa Ujerumani, Dar Es Salaam, na kabla ya kulima maeneo makubwa ya mimea ili kuwezesha kilimo cha muda mrefu(Permaculture) kufaulu, tulipaswa kuhakikisha kuwa wanaosaidia shambani, pamoja na watoto wetu , wana malazi mazuri watakapo fanya kazi kwenye mradi wao wa kilimo.
 
Msaidizi wetu mkuu, Tuzo, alikuwa tu na nyumba ndogo ya matope ambayo aliweza kujifichia iwapo jua ilikuwa kali.  Hatimaye, baada ya msimu wa Mvua (Februari hadi Mei) tuliweza kujenga nyumba mwafaka. Hii ni kwa uwezo wa michango mengi ambayo tulipokea.
 
Nyumba hii itakuwa na vyumba vitatu: chumba cha kulala na burudani, chumba cha zana na chumba moja ambapo tutakuwa na matumaini hivi karibuni kuwa na uwezo wa kuhifadhi mavuno yetu kutoka kwa shamba.

 

Zifuatazo ni baadhi ya picha za msingi wa jengo hilo. Katika picha moja, unaweza kuona nyumba ya matope. Kwa kweli, huu ni tofauti mkubwa ulioje!

Tungependa kuchukua fursa hii kuwapa wafadhili wetu wote  shukrani zetu kem kem, kwa mchango waenu mkubwa katika kampeni ya Kalenda. Asante sana!

Maelezo zaidi kuhusu shamba itafwata 😉

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *