2. Machi 2024

Umoja katika mabara – Familia ya Zebra inazidi kukua pamoja

TanZebras FC ndio timu rasmi ya heshima ya MSV Duisburg. Klabu ya mpira wa miguu ya Tanzania ni klabu ya jadi kutoka Meiderich, wanazidi kusonga mbele pamoja na kuipanua familia ya Zebra katika nchi mbali mbali. Cheti kiliwasilishwa kwa Don Mwakilambo, mwanzilishi mwenza na meneja wa Tanzebras , na Rais wa MSV Ingo Wald na Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi Markus Räuber katika Uwanja wa mpira wa Wedau. 
Hatua nyungine ilichukuliwa Julai tarehe 30, katika historia ya Tanzebras FC. Klabu ya mpira wa miguu pale Gongo La Mboto,
ambayo ilianzishwa na shabiki wa MSV Jörg Ahlbach, imekuwa sasa ni timu rasmi ya heshima ya klabu ya Meiderich.”Ni nini ambacho kinaweza kutoka kwa mkutano baina ya mtalii ambaye ni sapota wa MSV Duisburg na Mtanzania ambaye anapenda soka kwa moyo wa dhati?”Markus Räuber, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri alisisitiza.”

TZFC yalenga juu

Meneja wa TanZebras FC Don Mwakilambo na cheti rasmi.Klabu ya TZFC ilianzishwa mwaka wa 2014 tu, lakini mafanikio ambayo wamepitia hadi wakati huu ni wa kuvutia mno.  Baada ya kushindana katika ligi ya nne, waliweza kupandishwa kwenye ligi ya tatu, ambapo sasa hivi Tanzebras wanaingia mwaka wao wa pili. Ligi iko karibu kuanza, wiki si nyingi zijazo, na Timu ya Tanzebras nao wanajikakamua kwa udi na uvumba ili wawe tayari ligi litakapoanza. Kufikia sasa matokea yamekuwa ni mazuri tu.

Maendeleo ya TanZebras hayajaenda bila kutambuliwa na vyombo vya habari nchini
Taanzania. Shaffi Dauda, mwanahabari maarufu wa michezo nchini Tanzania,
huripoti mara kwa mara kuhusu TanZebras. Vile vile, magazeti makubwa nchini Ujerumani nao pia hawajawachwa nyuma ikija katika mambo ya kuripoti kuhusu Tanzebras.
Hutokosa pia kusikia maswali mengi yakiulizwa kila siku. Kwa sabau watu wanazidi kuulizia kuhusu timu ya Tanzebras, nayo sapoti inazidi kuongezeka. Kutoka Hamburg hadi Bavaria, kutoka Brussels hadi Berlin – TanZebras ipo katika midomo ya kila mtu.

 

“Soka haina mipaka”

Ushirikiano huu umeenda mbali zaidi ya upande wa michezo tu: “Ingawa Tanzebras ilianzishwa mwaka wa 2014, haijakuwa ni klabu ya mpira tu, bali imejihusisha pia na miradi mbali mbali ya kijamii ambayo mashabaki wa MSV pamoja na Tanzebras, wameungana mikono ili kuendeleza.

 Kwa hiyo, inatufanya tunajivunia sana kwamba sasa tunaweza kuongeza urafiki kati ya mashabiki wa MSV na TanZebras, ambayo imedumu kwa miaka mingi,
na sasa tunaweza pia kujumuisha urafiki rasmi kati ya vilabu,” alisema Räuber.
 Siku chache zilizopita,  TanZebras waliweza kukimbia katika kampeni za “Mbio za MSV,'” ampapo kilomita 600 ziliweza kukimbiliwa katika siku moja tu! 

Jörg Ahlbach, Mathias Langnickel na Don Mwakilambo katika ukabidhi.

Don alitumia siku kumi huko Duisburg kwa ajili ya kuwasilisha cheti,na pia alitumia fursa hii kukutana na wafuasi wengi kibinafsi.  Dhamana kati ya Duisburg na Dar es Salaam zimeimarishwa kwa mara nyingine. Hii ilikuwa pia mpangilio wa uwasilishaji wa sherehe za uwasilishaji wa cheti katika uwanja wa Wedau.

Ingo Wald na Markus Räuber walimpa Don mapokezi moto moto ambayo yalileta machozi mengi machoni mwa Don. Thomas Schöneberg, Mkuu wa Masoko katika MSV, naye alizungumza maneno ambayo yaliwagusa wote mioyoni.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *