13. Septemba 2024

Mipira Mpya ya TanZebras

Tumefurahia kuwaletea Derbystar, kama mshirika wa Tanzebras. Derbystar ni wanaspesheli katika uundaji wa mipira ya Bundesliga, na wataweza kutupa mipira mingi sana, ambazo zitatumwa Tanzania punde nafasi ya kuzituma itatokelzea.

Ahadi hii ya Derbystar inatupa motisha kuendelea na kazi hii yetu na tunafurahia sana kujiunga katika ustawishaji wa talanta ya wachezaji wachanga.

Kutokana na mfadhili wetu Inka Grings, uhusiano huu na Derbystar uliweza kudhibitishwa kutokana na meneja wao Joachim Böhmer . “Niliweza kusadiki Derbstar ili waweze kuungana nasi. Kampuni hii inasifa ya  kuunda vifaa bora. Kutokana na mipira hii, wachezaji wetu kule Dar es Salaam watakuwa na furaha tele wakicheza na mipira hii.” Grings alisisitiza.

 

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *