13. Septemba 2024

TanZebras wapata mafunzo ya kilimo cha muda mrefu (Permaculture)

Sophia na Franco wa Tanzebras hivi sasa wako Zanzibar wanahudhuria semina ya permaculture.  Maarifa ambayo watapata katika semina, wataenda kuwafunza wachezaji wenzao watakaporudi Dar es Salaam .

Hatua inayofuata ya kuwafanya wanatanzebras waweze kujitegemea imeshachukuliwa: Wachezaji wetu Sophia na Franco kwa sasa wanajifunza nguzo za msingi za kilimo cha muda mrefu(permaculture), ambazo  zitatumika kwenye mashamba ya TanZebras na pia kufunza wachezaji wa timu. Mavuno kutoka kwa kilimo cha mwaka mzima yatatengeneza chanzo kipya cha mapato kwa ajili ya TanZebras, ambayo yataweza kufadhili uendeshaji wa soka na kutekeleza miradi mengine. Mavuno ambazo zitavunwa zitauzwa  moja kwa moja ili kuimarisha uchumi wa eneo hilo.

Mafunzo katika nyanja ya uvumi endelevu ni sehemu ya dhana, ambayo inafanyika kwa ushirikiano na Ubalozi wa Ujerumani jijini Dar es Salaam. Kwa ajili ya ufadhili wa Ubalozi, kisima kirefu kwa sasa kinachimbwa shambani ili kuhakikisha usambazaji wa maji kwa shamba. Ili kuzingatia uendelevu,tumechagua kwa makusudi usambazaji wa nguvu
kutumia nishati ya jua, ambayo itasamabaza hasa nguvu za pampu ya maji.

Tungependa kuwashukuru wadhamini wetu na wafuasi wote ambao waliwezesha wachezaji wetu kuhudhuria semina hii ya hali ya juu sana na kupata maarifa mwafaka.  Vitendo hivi vizuri vinastawi tu tunakaposhirikiana pamoja!

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *